
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi akitoa salamu za mwisho kwenye ibaada ya kumuaga mama yake mzazi Desderia Mbilinyi.
Akizungumza wakati akisoma wasifu wa mama yake kwenye ibaada ya kumuaga na kumuombea katika kanisa Katoliki Muhimbili jijini Dar es salaam, Sugu amesema kuwa baada ya kuwekwa ndani afya ya mama yake ilibadilika na alianza kuugua shinikizo la damu lililozidisha tatizo alilokuwa nalo awali la figo.
Desderia alizaliwa Disemba 25, 1956 na maisha yake kwa sehemu kubwa alikuwa mkulima mdogo na amekuwa mjane toka mwaka 1992 baada ya mume wake kufariki na alikataa kuolewa tena na kujikita na shughuli za kanisa.
Desderia alifariki Jumapili ya Agosti 26 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu, ambapo anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake jijini Mbeya. Marehemu ameacha jumla watoto nane ambao watatu kati ya hao ni wa aliyekuwa mumewe na watano ni wanae aliozaa mwenyewe.