Sunday , 9th Sep , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Iringa,  Ally Hapi, amegoma kuzindua jengo la kliniki katika lituo cha afya cha Mgololo kilichopo Kata ya Makungu Tarafa ya Kasanga. 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi (katikati)

Hapi amegomea uzinduzi huo leo, wakati wa ziara yake inayoendelea katika Mkoa wa Iringa ya Tarafa Kwa Tarafa ambapo leo ametembelea Tarafa ya  Kasanga ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Baada ya kufika muda wa kuzindua Mkuu huyo wa Mkoa aligoma kwa kile alichodai ni kuwepo kwa harufu ya rushwa kutokana na kiasi cha fedha kilichotumika kwenye mradi kuwa tofauti na muonekano wa jengo lenyewe.

Hapi amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo, (TBA), Mkoani humo,  kuandaa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo ili ajiridhishe na baada ya kujiridhisha atarudi kuzindua au hatua nyingine zitachukuliwa endapo itabainika kuna ubadhirifu.