Monday , 2nd Jan , 2017

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka watumishi wote wa chuo cha ufundi Mirongo kilichopo Jijini Mwanza kuripoti na kusaini kitabu cha mahudhurio kwa katibu tawaka wa mkoa.

Mkuu wa MKoa wa Mwanza, John Mongella

 

Mongella amesema inashangaza sana kuona wafanyakazi wakipokea mishahara na kuishi kwenye nyumba za serikali wakati chuo hakifanyi kazi toka mwaka 2011 huku wafanyakazi wakihudhuria ofisini kila siku pasipokuwa na kazi ya kufanya tofauti na usafi tu jambo ambalo amesema haliwezekani.

Akizungumza na wafanyakazi wa chuo hicho Mongela amesema serikali  inatarajia kukifufua chuo hicho cha ufundi Mirongo ili kiweze kutoa wataalamu kwenye fani za ushonaji wa nguo, uchomeleaji na ufundi seremala lengo likiwa ni kusaidia vijana ili waepukane na makundi yasiyofaa.

Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1988 lengo mahususi likiwa ni kutoa mafunzo kwa walemavu kilifungwa mwaka 2011 kutokana na kukosa sifa za kimiundombinu ambapo licha ya kusikitishwa na uchakavu pia Mongela ameahidi kukirejesha chuo katika hali yake.

Sikiliza hapa:-