
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameahidi kutafuta shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kujenga mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kutatua changamoto ya uhaba wa mabweni ya wanafuzi wa chuo hicho.
Akiongea katika hafa ya uwekaji jiwa la Msingi wa Jengo Jipya la Maabara ya Kisasa linalojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China, rais Dk. Magufuli amesema hata hivyo anatoa fedha hizo kwa sharti ujenzi wa mabweni hayo ufanywe kwenye eneo la hapo hapo chuoni.
Aidha, Dk. Magufuli amewashauri wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuacha kujenga majengo katika maeneo mengine ambayo wakati mwingine yanakosa hata wapangaji wa kutosha, na badala yake wasaidie katika kujenga mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kuna wapangaji wengi ambao ni wanafunzi.
Hata hivyo Rais Dk. Magufuli hakusita kuwaasa wanafunzi wa hao wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kuwaeleza kuwa wamekuja chuoni kusoma, hivyo wazingatie masomo na waachane na siasa ambazo kama wanazihitaji watazikuta tu wakishamaliza elimu yao.