Friday , 1st Apr , 2016

Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa umma wa taifa hilo jana imekatishwa kwa kelele zilizopigwa na baadhi ya wabunge wa bunge la nchi hiyo. Kitendo hicho kilimlazimisha rais Kenyatta kuacha kuzungumza na kumwachia Spika wa Bunge kuendelea.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Kitendo hicho kinatajwa kuwa cha kwanza cha aina yake kufanyika tangu 2008, pale ambapo bunge lilivurugika kutokana na kelele na maneno makali baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika Desemba 2007.

Lakini awali upande wa upinzani ulionesha dalili za kuvuruga hotuba hiyo lengo lao likiwa kuonesha kutoridhishwa kwao na serikali ya Kenyatta.

Spika wa Bunge Justin Muturi aliamuru wana usalama kuwaondoa wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakichochea vurugu hizo.