Tuesday , 12th Mar , 2019

Baada ya makundi mbalimbali nchini Algeria kuandamana kumpinga Rais wa nchi hiyo kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, hatimaye Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo kwa muhula wa 5.

Sanduku la kura

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya jopo la majaji kutangaza nia ya kutosimamia uchaguzi endapo Rais Abdelaziz Bouteflika atatangaza nia tena ya kugombea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Algeria kiongozi huyo ametangaza kutogombea tena kwa muhula wa tano licha ya awali alipokuwa kwenye matibabu nchini Switzerland kutangaza kugombea nafasi hiyo.

Uchaguzi huo ulipaswa kufanyika Aprili 11 2019, lakini Rais huyo alitangaza kuwa atazungumza na umma kwa ajil ya kutangaza tarehe rasmi ya nchi hiyo kufanya uchaguzi.

Hivi karibuni makundi ya wanafunzi nchini walilazimika kupewa likizo ya mapema kufuatia mfululilzo wa maandamano ya kumpinga Rais huyo.