Monday , 7th Mar , 2016

Serikaliya Tanzania imesema inakusudia kutuma timu ya wataalamu kwa ajili ya kukagua na kufanya tathimini ya kupata gharama ya fedha halisi zilizotumika wakati wa ujenzi wa gati ya bandari ya Pangani mkoani Tanga.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Prof. Makame Mbarawa,

Hatua hiyo ya ukaguzi inatokana na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Prof. Makame Mbarawa,baada ya kutilia shaka mradi wa ujenzi wa gati hiyo alipotembelea eneo hilo katika ziara yake Mkoani Tanga.

Prof. Mbarawa amesema kuwa Hadidu rejea zitaiongoza timu hiyo katika ukaguzi wake na kuangalia thamani halisi ya fedha kama kweli imeendana na mradi husika.

Ujenzi huo wa gati hiyo unaotekelezwa na Kamapuni ya Alpha Logistic unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.3za Kitanzania hadi kukamilika kwake na ulianza na kutekelezwa mwaka 2014 na ulitakiwa kukamilika mwishoni mwa desemba mwaka jana.