Thursday , 1st Dec , 2016

Serikali imesema bado kuna changamoto kubwa katika sekta ya misitu hasa uvunaji haramu na usafirishaji wa magogo nje ya nchini kinyume na sheria pamoja na ukataji miti ovyo usiokuwa na mipaka ambao unailetea madhara makubwa kwa nchi.

Prof. Jumanne Maghembe

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa badala ya magogo hayo kusafirishwa nje ya nchi ni vyema yakachakatwa hapa nchi ili watanzania waweze kujiajiri kwa kutengeneza vitu mbalimbali vya samani kupitia magogo hayo kuliko kusafirishwa nje ya nchi bila kuchakatwa.

Aidha, Prof. Maghembe amebainisha kuwa ili kuepuka shughuli za binadamu kuingia kwenye maeneo ya hifadhi kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuhakikisha sekta binafsi kupanda misitu midogo midogo kwenye maeneo husika.