Thursday , 3rd Apr , 2014

Jeshi la polisi mkoani Tabora limewataka wakazi wa mkoa huo kuacha tabia iliyojengeka hivi karibuni ya kujichukulia sheria mkononi kwa kutowahukumu watuhumiwa wa makosa mbali mbali.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishan Msaidizi wa Polisi Juma Bule ametoa wito huo leo wakati akiongea na East Africa Radio ambapo amewataka wananchi kuripoti katika vyombo vya dola matukio yote yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Kaimu kamishna Bule ametoa wito huo kufuatia mapigano ya kugombea ardhi baina ya wakulima na wafugaji katika eneo la mpaka kati ya wilaya za Kishapu mkoani Shinyanga na Igunga mkoani Tabora ambayo yameua watu watano.