
Augustino Mrema - Mwenyekiti Bodi ya Parole
Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.
"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema
Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.
"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.