Tuesday , 2nd Feb , 2016

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata wahamiaji haramu 12 raia wa nchini Ethiopia.

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata wahamiaji haramu 12 raia wa nchini Ethiopia wakiwa kwenye gari aina ya Noah yene namba za usajiri T 786 BHZ wakisafirishwa kwenda mjini Tunduma mkoani Mbeya kwa ajili ya kwenda nchini Afrika ya Kusini.

Akitoa tarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema wahamiaji hao wamekamatwa na jeshi la polisi majira ya saa nane usiku katika eneo la mikumi barabara ya Morogoro-Iringa.

Kamanda Paulo ameeleza kwamba baada ya wahamiaji hao kuhojiwa wamesema walitokea mjini Adis ababa Ethiopia wakielekea nchini Afrika ya Kusini na kwamba dereva na kondakta wa gari lililokuwa likisafirisha wahamiaji hao wanaendelea kuhowa.

Naye dereva wa gari hilo Kim Mustapha amesema aliagizwa na mwaajiri wake kupeleka wahamiaji hao mkoani Mbeya ingawa hakujua kama ni wahamiaji haramu….

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia matukio ya kukamatwa wahamiaji haramu nchini mara kwa mara wamevitupia lawama vyombo vya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi kutoimarisha ulinzi mipakani ambapo wamemshauri Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya maafisa wa uhamiaji na jeshi la polisi hasa wanaohusika kulinda mipaka ya nchi.