Monday , 22nd Jun , 2015

Jeshi la polisi mkoani kagera limefanikiwa kukamata raia  watano wa kigeni  kutokea  nchi za  Elitria na Ethiopia walioingia nchini kwa njia haramu.

Wahamiaji haramu waliokamatwa Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumkamata raia watano wa kigeni wanao dhaniwa kuwa wametokea nchi za Eritrea na Ethiopia waliopitia nchini Uganda na kuingia mjini Bukoba bila kufuata taratibu zinazohusika kwa kusingizia wanakwenda kufungua hoteli ya kimataifa jijini Dar es salaam huku wakiwa na dola 2500 mfukoni.

Akiongea mjini Bukoba kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Gilles Mloto amesema jeshi la polisi liliwatilia mashaka raia hao wa kigeni mara baada ya kuwakuta katika basi la Sumri lililokuwa likitokea mkoani Kagera likielekea jijini Dar es salaam na baada ya kufika katika kizuizi wilayani Biharamulo basi hilo lilikaguliwa na kubainika limebeba raia wa kigeni watano ambao sasa wamefikishwa katika kituo cha polisi mjini Bukoba kwaajili ya upelelezi zaidi.

Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Gilles Mloto amesema raia hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili taratibu za kisheria ziweze kufuatwa .

Katika katika tukio jingine jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina short-gun ambazo zilikuwa zikitumika kufanya uwindaji haramu katika pori la akiba la kimisi na kwamba majingili waliokamatwa na silaha hizo pia walikutwa na mnyama aina swala ambaye walikuwa wamemuuwa katika pori hilo lililopo wilayani Karagwe.