Tuesday , 24th Jan , 2017

Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CUF, kwa mara ya kwanza amezungumzia kile alichokita "kukataliwa" kwa Chama cha Wananchi CUF katika maeneo mbalimbali hasa Zanzibar huku akikielekeza jinsi ya kumpata "Mchawi" wake

Polepole (Kulia), Nembo ya CUF (Kushoto)

Polepole akizungumza na waandishi wa Habari, leo Jijini Dar es Salaam kuhusu matokeo ya chaguzi ndogo za ubunge na udiwani, amesema mchawi wa CUF yumo ndani ya CUF na kukishauri chama hicho kumtafuta mchawi huyo ndani ya CUF hasa visiwani Zanzibar badala ya kusingizia watu wengine walio nje ya CUF na kutoa lawama kwa CCM.

Amesema matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Dimani Zanzibar yanadhihirisha jinsi ambavyo wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakikikataa chama hicho, na badala yake kuzidi kukipenda Chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ushahidi wa hilo ni takwimu za matokeo ya ubunge katika jimbo hilo.

"Tumekuwa tukilaumiwa sana na CUF, sasa matokeo ya Dimani yanadhidirisha kuwa tatizo ni CUF, tumefanya utafiti mdogo na tumeona kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, CUF ilipata kura 2300 hivi, lakini uchaguzi huu kimepata kura takriban kura 1200, hili ni anguko la zaidi ya asilimia 50 kutoka uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Dimban mwaka 2015. CCM mwaka 2015 kilipata kura  4400, na sasa tumepata kura zaidi ya 4800, hilo ni ongezeko, kwahiyo CUF imtafute mchawi kulekule CUF na hasahasa kule Zanzibar." Amesema Polepole

Katika uchaguzi wa jimbo la Dimani, CCM ilimepa kura 4,860, sawa na asilimia 78.74.