Friday , 24th Jun , 2016

Kamishna wa jeshi la zimamoto na uokoaji, Thobias Andengenye amewataka wananchi kote nchini kuheshimu kazi inayofanywa na jeshi la zimamoto hasa kwa kupisha magari hayo pindi wananchi wanapoyaona ili yaweze kuwahi katika maeneo ya majanga

Andengenye ameyasema hayo Jijini Dar es salaam na kusisitiza kwamba jeshi lake hupata wakati mgumu wakati wa matukio ya moto kwa baadhi ya watu kushindwa kupisha magfari hayo kwa kutojali yanakokimbilia.

''Ukiona gari la zimamoto jamani jaribu kuona kama ndiyo nyumba yako inaungua, fanya namna upishe gari hilo mara moja liwahi kwenye tukio likaokoe mali na nyumba''- Amesema Kamanda Andengenye.

Aidha Kamanda amewataka wananchi wanapojenga nyumba zao kuhakikisha wanaheshimu kuacha njia za kupita yanapotokea majanga ili magari yaweze kupenya kirahisi kufika maeneo yenye matatizo