Msemaji wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, amesema hawakukurupuka kuendesha operesheni hiyo, bali hakuna mgeni anayeruhusiwa kufanya kazi nchini bila vibali.
Tamko hilo la kusisitiza limekuja huku takwimu zikionesha kwamba, hadi mwishoni mwa wiki, watu 79 walishakamatwa na Idara ya Uhamiaji kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo.
Aidha Bw Nantanga amewataka waajiri wote kuhakikisha raia wote wa kigeni waliowaajiri wanafanya kazi kihalali. Amesisitiza, endapo kuna raia wa kigeni asiye na kibali au yuko kinyume cha sheria, asalimishwe Uhamiaji mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake, au kuwasili sha taarifa zake.

