Friday , 12th Feb , 2016

Nyumba za wananchi za Kilimani Zanzibari zipo hatarini kudidimia na kuchukuliwa na bahari kutokana na mabadililo ya tabia nchi huku serikali ya muungano ikiahidi kuchukua hatua za makusudi za kuzinusuru na uharibifu huo.

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina

Msimamo huo wa serikali umetolewa na Naibu waziri wa Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga mpina baada ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na uharibifu mkubwa eneo la kilimani uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Kutokana na hali hiyo Wananchi wengi wameathirika kutokana na hivi sasa kukosa kufanya kilimo na pia sehemu za michezo ambazo hivi sasa zimetoweka kutokana na kumezwa na bahari.

Mhe. Mpina amesema kwa sasa anataka wahusika waweze kupanda mikoko katika eneo hilo ikiwa serikali ipo kwenye mchakato wa kujenga matuta ya kukinga maji ambayo yatagharibu zaidi ya bilioni moja 1.2

Hapo awali Mkurugenzi wa Mazingira wa Zanzibari, Juma bakari Alawi amesema mabadiliko ya tabia nchi ya tabia nchi yanahatarisha eneo hilo na endapo hatua za haraka hazitachukuliwa litageuka kuwa bahari na kuhatarisha maisha ya Wananchi na maendeleo ya nchi.

Naibu Waziri Mpina anakuwa raisi wa Kwanza anaeshughulikia masuala ya muungano kutembelea visiwa hivyo na kutoa ahadi za utekelezaji wa utunzaji wa Mazingira.