Wednesday , 4th Mar , 2015

ZOEZI la uandikishaji wa daftari la kudumu la kupigia kura kwa mfumo wa kibaiologioa (BVR) limemalizika katika halmashauri ya mji Makambako katika kati tisa na kuendelea kwa wiki mbili katika kata za pembezoni za halmashauri hiyo.

Wananchi wakiwa wamejitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi wa halmashauri ya mji Makambako Vumilia Nyamoga amesema kuwa zoezi hili katika kata tisa za makambako mjini zimekamilika na zoezi limefungwa na kuwa litaendelea katika kata za Kitandililo ambako zoezi lilianza juzi.

Amesema kuwa kata zingine ambako zoezi litaanza siku ya leo ni kata ya Mahongole ambapo litaendeshwa kwa wiki moja na kuwa katika kata ya Utengule zoezi litaendeshwa wiki moja baada ya kumalizika kata hizo mbili.
Amesema kuwa zoezi hilo baada ya kuongezwa siku mbili za Jumatatu na Jumanne limeendelea vizuri na kuwa watu katika siku ya kwanza watu walijitokeza kwa wingi na siku ya pili ambayo ni jana watu walipungua kabisa.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Makambako, Chesco Mfikwa amesema kuwa zoezi hilo kwa siku hizo mbli wananchi waliendelea kujitokeza na kuwa siku ya mwisho ya nyongeza wananchi walijitokeza wachache tofauti na siku ya kwanza ya nyongeza.

Amesema kuwa mpaka kufikia siku ya juzi walikuwa wamewaandikisha wakazi 44,227 wa kata tisa ambazo zoezi hilo lilianzia.

Amesema kuwa wameanza katika kata ya Kitandililo ambako kwa sasa wanafanya shughuli za uhamasishaji wa wananchi kuja kujiandikisha ili waweze kujitokeza kwa wingi kwa muda wa wiki moja waliyo wekewa wakati wa kata hiyo na zingine.

Amesema kuwa zoezi hilo katika halmshauri yake kuna wiki mbili zimebaki ili kufungwa na kuelekea katika halmshauri zingine.

Mwandishi amepita katika baadhi ya vituo vya uandikishaji majira ya saa saba na saa nane mchana kwa siku ya jana na kuona kuwa wananchi wanao hitaji kujiandikisha tofauti na siku chache zilizo pita ambapo kulikuwa na wananchi wengi katika vituo.

Mmoja wa waandikishaji katika kituo kimoja katika kata ya mjimwema amesema kuwa kwa siku mbili walizo ongezewa kuna wananchi 115 kwa siku ya kwanza na siku ya pili kufikia saa saba walikuwa na watu 50 walio waandikusha na kuwa wamekaa katika kituo hicho kwa muda zaidi ya masaa 3 bila kuja mtu kuandikisha.