Friday , 13th Nov , 2015

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),limesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na taaasisi ya utafiti ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na kusini(ESAURP),katika utafiti na ujengaji uwezo wa wafanyabiashara wadogo na wa kati(SME)

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa

Makubalino hayo yalifanyika jana jijini Dar es salaam chini ya katibu mtendaji wa NEEC, Bi. Beng'i Issa na Mkurugenzi wa ESAURP, Prof. Tedi Maliyamkono huku wakisema lengo ni kusaidia wafanyabishara wadogo na wakati wapatao milioni 3.

Akizungumza katika hafla hiyo Bi. Beng'i amesema biashara za aina hiyo inachipukia kila siku lakini tatizo biashara nyingi za aina hiyo zipo katika sekta isiyo rasmi kwa hiyo zinakosa uwezeshaji na serikali inakosa mapato kwao.

Issa amesema makubaliano hayo yatakuza na kurasimisha biashara hizo kwa njia ya uwezeshaji na kufafanua kuwa, ushirikiano huo umejikita katika tafiti na kujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogo kwa kuwaongezea ujuzi wa biashara.

Kwa upande wake Prof. Maliyamkono amesema kuwa ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania na serikali kwa ile ESAURP, inafanya tafiti katika suala la kukuza ajira ambazo nyingi zinatokana na biashara ndogondogo.