Wednesday , 14th Sep , 2016

Ndege mbili zilizokuwa zimebeba mirungi zimewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu baada ya kuzuiwa kwa muda wa wiki moja.

Mirungi

Wiki iliyopita ndege za Kenya zilipigwa marufuku kupeleka mirungi nchini Somalia jambo ambalo lilianza kuleta mdororo wa soko la zao hilo nchini Kenya.

Bado haijajulikana ni kwanini Somalia ilipiga marufuku, lakini iliondolewa siku ya Jumanne jioni baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.

Aidha kwa biashara ya kawaida ndege zaidi ya 15 hutua nchini Somalia kila siku zikiwa zimebeba mirungi