Thursday , 16th Jul , 2015

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania Al-Haji Bulembo, amemshauri katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye aviite vyombo vya habari ili afute kauli ya kwamba chama hicho kitashinda hata kwa Goli la Mkono.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Taifa Alhaji Abdallah Bulembo

Akiongea na East Africa Radio leo Mwenyekiti huyo amesema viongozi wawe wanaangalia kauli wanazozitoa wakati wanaongea na wananchi au waandishi wa habari kwa kuwa maneno mengine huwa yanatafsiriwa tofauti na jamii.

Al-Haji Bulembo ameongeza kuwa Ndugu Nape asichanganye Siasa kwa mifano ya Simba na Yanga kwa kuwa vitu hivyo ni tofauti huku akisema kuwa Katibu huyo mwenezi anafanya kazi yake vizuri kwa kuteleza kwa binadamu ni jambo la kawaida.

Bulembo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kina uhakika wa kushinda na kwenye uchaguzi sio kama mchezo wa mpira ila masanduku ya kura ndiyo yatakay amua ni nani atakaye chukua uongozi.