Waziri Nchemba amesema hayo akizindua zoezi la kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa na kugawa vitambulisho katika mkoa wa Tabora na kukagua zoezi hilo linavyoendelea kwasasa.
Mh. Waziri amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .
"Zoezi hili ni bure kujiandikisha na kupata kitambulisho pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomu za kujiandikisha na wala zoezi hili lisiunganishwe na siasa."amesema
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa vitambulisho vya Taifa, Andrew Masawe amesema zoezi la kuandikisha wananchi linatakiwa kuisha ifikapo Disemba 2018 na mpaka sasa mikoa 19 imeshaanza kuandikisha wananchi kupata kitambulisho cha utambuzi, huku mikoa ya Mara, Arusha , Mwanza Simiyu na Ruvuma ikifanya vizuri katika uandikishaji wananchi.

