Baada ya makabidhiano hayo mwenge huo umeanza mbio zake katika Mkoa wa Songwe ambapo unatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.7.
Mbio hizo zimeanza katika mkoa huo kwa kuzindua mradi wenye lengo la kufundisha vijana kilimo katika kijiji cha Kanga ambapo vijana mbalimbali wanatarajia kunufaika na mradi huo.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu George Jackson Mbijima amewataka vijana kuchangamkia fursa za ajira za kilimo vijijini na kuacha kudanganyika na kazi zisizo na uhakika ambazo huenda kuzitafuta mijini.
''Eneo ambalo linasababisha ajira nyingi katika nchi yetu ni kilimo, nataka kuwashauri vijana wenzangu kujiingiza kwenye kilimo kwani ndiyo yenye ajira ya uhakika''- Amesema Mbijima.

