Mbunge wa jimbo la Kyela Dk Harison Mwakyembe
Uongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa jimbo la Kyela Dk Harison Mwakyembe umebainisha hayo ulipomkaribisha mfanyabiashara maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki, Gagan Gupta kuangalia fursa zilizopo ndani ya wilaya hiyo.
Akizungumzia ujio wa mfanyabiashara huyo ambaye ndiye mmiliki wa viwanda vya Kamal vya kuzalisha Chuma Afrika Mashariki Dk Mwakyembe amesema huo ni mwanzo wa kuwaleta wawekezaji kujionea fursa zilizopo hususani katika kilimo cha zao la Mpunga.
Dk Mwakyembe amesema baada ya kumtembeza mwekezaji huyo na kubaini fursa zilizopo,ameonesha nia ya kuja kuwekeza kiwanda kikubwa cha usindikaji zao la Mpunga.
Kufunguliwa kwa milango ya uwekezaji wilayani hapa ni fursa nyingine ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla.