Thursday , 2nd Jun , 2016

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewataka wataalam wa Maabara, Ustawi wa Jamii na Wahudumu wa Afya, waanze kutumia muongozo wa namna ya ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya ushahidi wa kimahakama kwa waliofanyiwa ukatili.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewataka wataalam wa Maabara, Ustawi wa Jamii na Wahudumu wa Afya, waanze kutumia muongozo wa namna ya ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya ushahidi wa kimahakama kwa waliofanyiwa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ali Mohamed, ametoa kauli hiyo hii leo alipokuwa akizindua muongozo huo na kubainisha kuwa hapo awali ilikuwa ngumu kupatikana ushahidi lakini mwongozo huo utasaidia kukusanya ushahidi na kumaliza kesi za ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Ayoub Mwenda amesema kuwa muongozo huo utawasaidia katika ukusanyaji wa ushahidi na utapunguza gharama za uendeshaji wa kesi za ukatili hivyo utarahisisha katika upatikanaji wa haki kwa waathirika wa ukatili.