Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Aziz Msuya
Dkt Aziz amebainisha kuwa walitoa agizo kwa wafanyabiashara hao wafunge biashara zao kwa muda mpaka pale ugonjwa wa kipidupindu utakapoisha lakini wafanyabiashara hao wameonesha kukaidi agizo hilo.
Kauli hiyo wa Dk. Msuya ameitoa jana wakati idadi ya wagonjwa wa kipindupindu katika kambi ya Mburahati ikiwa ni 45 na siku ya leo pekee wamepokea wagonjwa 22 ambao wametoka maeneo yaleyale yanayoripotiwa kutoa wagonjwa wengi.
Dkt.Aziz Msuya amesema Jana waliwaruhusu wagongwa 22 na kubakiwa na wagonjwa 23 na baadae kuongezeka 22 na idadi kubakia palepale,hali inayotokana na wananchi kutofuata maagizo ya serikali ya kuacha kuuza vyakula kiholela.

