Saturday , 10th May , 2014

Mke wa waziri mkuu wa Tanzania Mama Tunu Pinda amewataka wazazi hapa nchini wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi wasiogope kuwapeleka watoto hao shule kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.

Tunu Pinda, mke wa Waziri mkuu wa Tanzania

Mke wa waziri mkuu wa Tanzania Mama Tunu Pinda amewataka wazazi hapa nchini wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi wasiogope kuwapeleka watoto hao shule kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.

Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea msaada wa vitabu mbali mbali kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi, Mama Tunu Pinda pia ametoa wito kwa shule zenye watoto hao kuhakikisha zinatoa upendeleo maalum ili waweze kusoma kama watoto wengine.