Wednesday , 22nd Jul , 2015

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi anakusudia kuzishawishi taasisi za kifedha kufunga kamera za ulinzi (CC-TV Camera) ambazo zitakuwa na mawasiliano ya kiusalama baina ya benki husika na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.

Kamanda Msangi ametoa rai hiyo wakati akipokea msaada wa kompyuta mbili za kisasa zenye thamani ya Shilingi milioni 4 kutoka Benki ya Tanzania Investment (TIB) tawi la Mbeya kwa ajili ya matumizi ya jeshi hilo.

Amesema katika kuimarisha ulinzi kwenye taasisi za kifedha ni vyema kukafungwa kamera maalumu (CC-TV Camera) nje ya benki ambazo zitakuwa zina mawasiliano ya moja kwa moja na jeshi hilo.

Aidha amesema kuwa hiyo itasaidia kwa polisi kutambua jambo lolote linaloweza kujitokeza benki husika na kutoa msaada kwa haraka zaidi, ambapo polisi watakuwa na uwezo wa kuwaona watu wanaoingia na kutoka kila benki kwa wakati mmoja.

Kwa upande wake mdau wa taasisi za kifedha, meneja wa Benki Tanzania Investmen.

(TIB) tawi la Mbeya, Hemed Sabuni amesema ni jambo zuri kuweka mfumo wa kisasa wa kiusalama ili kurahisisha utendaji kazi kwa jeshi la polisi.