
Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakiwa na mwenyekiti wa EAC, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli. (Picha: maktaba)
Mkutano huo una lengo la kujadili namna ya kutekeleza mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya(EPA).
Mkutano huo wa viongozi wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unatarajiwa kuhudhuriwa na mwenyeji wa mkutano huo Rais Dkt. John Magufuli, Rais Yoweri Museven wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na nchi nyingine zitawakilishwa na mawaziri.
Wakati mkutano huo ukitarajiwa kuanza tayari nchi za Kenya, Rwanda na Uganda, zimekwishasaini mkataba huo wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara huku Tanzania ikikataa kufanya hivyo kwa madai kuwa mkataba huo utaizuia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda kwa kukuza uchumi wake.