
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu nchini Tanzania,Benjamin Wiliam Mkapa amesema Rais wa awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere alifanikiwa kujenga misingi imara ya kielimu hali iyowezesha wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuondokana na ujinga hali inayotakiwa kuendelezwa.
Hayo ameyaeleza leo na rais mstaafu Mkapa wakati akifungua Kongamano la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam likishirikisha Wanataaluma mbalimbali pamoja na wanafunzi.
Kongamano hilo linalenga kujadili Misingi mbalimbali ya maendeleo iliyoasisiwa na Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere,wakati wa harakati za kutafuta uhuru na baada ya uhuru wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Mhe. Benjamin Wiliam Mkapa akizungumza katika Kongamano hilo amesema Mwalimu Nyerere alifanikiwa kuwekeza katika Elimu na kuwapa fursa sawa wananchi wake kupata elimu.
Mkapa ameongeza kuwa Mwalimu Nyerere amekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi nyingi za Afrika zinapata uhuru ili kuwa na mshikamano wa bara la Afrika huku sera ya ujamaa ilimpa fursa ya kuwaunganisha wananchi licha ya kuruhusu wananchi wanaosaka maendeleo hayo kwa ajili ya wote.