Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba
Miswada iliyopitishwa hii leo ni wa Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi, Muswada wa uwazi na uwajibikaji katika cuhimbaji wa gesi na mafuta huku Mswada wa sheria na mafuta na gesi hapo jana.
Akijibu hoja za wabunge waliochangia Muswada huo Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuzuia kupitishwa kwa miswada hiyo ni ucheleweshaji wa maendeleo kitu ambacho hakikubaliki kwa taifa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima amesema kuwa suala la kupitishwa kwa miswada hilo ni la kitaifa na linajumuisha pande zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar na kuwatoa wasiwasi wananchi wa Zanzibar juu ya Muswada huo.
Aidha Mh. Malima amesema nchi inayokwenda na uwekezaji lazima iwe na miongoz pamoja na sera zinazofata sheria ambazo zitaweza kuwapa muongozo wawekezaji na kuleta tija ya maendeleo kwa taifa.
Katika hatua nyingine katika kupitisha muswada mwingine wa uwazi na uwajibikaji katika Uchimbaji wa gesi na mafuta, waziri wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene amesema kuwa kusipokuwepo na uwazi katika kulinda rasimali hizo ni watu wachache wataweza kufaidika na rasilimali hizo.