Thursday , 2nd Jun , 2016

Taasisi za umma nchini zimetakiwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao eGA katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA serikalini ili kurahisisha mpango wa kubaini na kuondoa urudufu na kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji mifumo.

Taasisi za umma nchini zimetakiwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao eGA katika kupanga na kutekeleza miradi ya TEHAMA serikalini ili kurahisisha mpango wa kubaini na kuondoa urudufu na kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji mifumo inayofanana ndani ya serikali.

Taarifa iliyotolewa na meneja habari, elimu na mawasiliano wa wakala wa serikali mtandao Suzan Mshakangoto ambaye amesema kuwa taasisi yoyote ya umma inayotaka kuanzisha mradi wa TEHAMA inatakiwa kuwakilisha mradi huo ukiwa unaendana na vigezo vilivyowekwa katika orodha hakiki ya miradi ya TEHAMA serikalini.

Aidha wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi ya utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini wanashauriwa kufuata orodha hakiki hiyo ili kujua mahitaji halisi ya serikali na kuweza kujenga mifumo ya TEHAMA endelevu na inayoleta tija kwa umma.