Monday , 14th Mar , 2016

Miili ya watu wawili kati ya watatu waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa JW unaomilikiwa na kampuni ya Tanzanite One,Mkoani Manyara imepatikana na utafutaji wa mwili uliosalia unaendelea.

Wafanyakazi wa machimbo ya JW wakiwa katika harakati(Picha na Maktaba)

Akizungumzia tukio hilo mchmbaji mmoja alienusurika kufa, Benendict Gidishi, amesema kuwa wachimbaji hao walizama katika mgodi huo kwa muda wa siku tano kinyemelea lengo likiwa ni kutafuta madini.

Kwa upande wake Mmoja wa waokoaji wa machimbo hayo Mahmud Juma amesema zoezi lilikua kugumu kuweza kufanikisha kutokana na watu hao kubwana na kifusi hicho ambacho kiliwaangukia wakati wakiwa katika zoezi la kuchimba.

Wachimbaji waliopotea ni mmoja aliyejulikana kwa jina la Hemed, huku wengine wakiwa ni Saidi Mgosi, pamoja na Khalidi Juma.