Wednesday , 14th Sep , 2016

Serikali imesema migogoro ya ardhi ni suala linalohitaji muda wa kutosha na mipango maalum ya kuitatua kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa nchini hali itakayofanya kuweka mipango ya miaka mitano ili kuimaliza.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kutokana na ukubwa wa tatizo, migogoro hiyo itaendelea kuwepo na serikali itakuwa inaishughulikia kwa njia za kisayansi.

Mhe. Lukuvi amesema kutokana na hali hiyo serikali imejiwekea lengo na mikakati madhubuti kwa kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano ni lazima wawe wameimaliza na pande zinazohasimiana ziridhike kutokana na utatuzi utakofanyika.