Friday , 25th Nov , 2016

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula amesema mgogoro wa ardhi wa eneo la Chasimba Wazo Hill Jijini Dar es Salaam umemalizika na kinachoendelea kwa sasa ni hatua za urasimishaji ardhi kwa wakazi wa eneo hilo.

Angelina Mabula

 

Mh. Mabula ameyasena hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio ilipotaka kujua hatua gani zimechukuliwa na serikali katika kuhakikisha wanamaliza mgogoro baina ya mmiliki wa kiwanda cha Wazo Hill na wananchi wa maeneo hayo na kuwa utaratibu kama huo unaendelea katika maeneo mengi yenye migogoro ya ardhi.

Amesema hatua ya urasimishaji ni maafikiano yanayojumuisha wananchi wa eneo husika na wataalamu wa ardhi ili kutenga maeneo ya huduma muhimu yasivamiwe na kupunguza usumbufu ambao kama hautazuiliwa mapema unaweza kusababisha usumbufu kwa jamii inayozunguka maeneo hayo.