Saturday , 1st Oct , 2016

Kiongozi wa mbio za Mwenge nchini George Mbijima amekemea vikali hali ya mauaji ya kikatili yanayofanyika kila mwezi katika wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge George Mbijima

Akizungumza na mamia ya wananchi wakati wa mbio za Mwenge katika wilaya hiyo Mbijima amepokea taarifa iliyoonyesha kwamba kila mwezi watu watatu wanauawa kwa matukio ya kishirikina jambo ambalo halikubaliki kwa mujibu wa sheria.

“Haiwezekani manispaa ina kambi zaidi ya tano watu wanatumia silaha hovyo, mauaji yanatokea ya wananchi wasio na hatia ni wajibu wa kila mmoja kushirikiana na serikali katika kulind usalama wa nchi” Amesema Mbijima.

Mwenge wa Uhuru ulifika mkoani Tabora ukitokea mkoani Singida ambapo umezidua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuhimiza shughuli za maendeleo na kuchochea utulivu na amnai ya nchi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Mbijima amewataka watu wanaomiliki silaha kuzisalimisha kwa jeshi la polisi mara moja kabla hatu za kuwabaini hazijafanyika.