Maalim Seif amesema mara kadhaa amefanya juhudi za kuwasiliana na wakuu wa usalama lakini wamemtaka kwanza kupitia kwa Waziri wa nchi aliye katika Ofisi ya makamu wa pili wa Rais jambo ambalo limemshangaza yeye kwani ni kinyume cha protokali Makamu wa Rais kuomba ruhusa kwa Waziri.
''Nimeongea pia na Rais Shein wa Zanzibar pamoja na makamu wa pili Balozi Seif Ali Idd lakini wote wamesema hawajui lolote kuhusu kundi hilo linalowashambulia wapinzani''Amesisitiza Maalim Seif
Chama cha CUF kimeendelea kusisitiza kuwa kilishinda katika uchaguzi uliopita na hivyo hakitashiriki katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 20 Machi na Serikali iache kufanya hujuma zitakazoivuruga nchi.





