Monday , 21st Mar , 2016

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam DSE yameshuka kwa asilimia 34 kutoka shilingi bilioni 7. 2 ilivyokuwa juma lililopita hadi shilingi bilioni 4.8 kwa mujibu wa takwimu za mauzo katika soko hilo kwa kipindi cha juma moja lililopita.

Afisa Mauzo wa Soko la Hisa la Dar es Salaam DSE Bi. Mary Kinabo.

Afisa Mauzo wa Soko hilo Bi. Mary Kinabo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo na kwamba katika kipindi hicho, idadi ya hisa zilizouzwa nayo imeshuka kwa asilimia 39 kutoka hisa milion 1.9 hadi hisa laki saba.

Bi. Kinabo ameongeza kuwa hata mtaji wa soko haujaongezeka katika kipindi hicho na badala yake umebakia kiasi kilekile cha mtaji wa shilingi trilioni 21 kwa makampuni ya nje na shilingi trilioni 9 kwa makampuni ya ndani.

Aidha Afisa Mauzo huyo wa DSE amesema kushuka kwa mauzo hayo ni hali ya kawaida kwani inatokana na mwenendo wa soko kulingana na mahitaji na mauzo ya hisa kwa kipind husika.