
kwa mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.
Miongoni mwa shule zilizokumbana na kadhia hiyo ya kufutwa kwa matokeo hayo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopoHalmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji, Shule za Msingi za halmashauri ya Chemba ambao viongozi wake walitajwa kuhusika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema “Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Fountain of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo. Amesema Charles Msonde.
Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.
Septemba 26, 2018 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hazina iliyopo Magomeni, Dar es salaam, Patrick Cheche (43) na walimu wenzake walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kupata mitihani na kutoa maudhui ya mitihani hiyo kwa watahiniwa wa darasa la saba isivyo halali.
Akiwasomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono aliwataja washtakiwa hao kuwa ni mwalimu Laurence Ochien (30), mkazi wa Magomeni Makuti
Wengine ni mwalimu Justus James (32) Mkazi wa Kimara Mwisho Mavurunza, Nasri Mohammed (32) Mkazi wa Magomeni Makuti. Kombakono katika shtaka la kwanza amedai Septemba 4, 2018 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wote kwa pamoja walikula njama kwa kuingilia mitihani ya taifa ya darasa la saba isivyo halali.