Sunday , 21st Jul , 2019

Kufuatia kutenguliwa nafasi ya kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, January Makamba ametoa kauli yake.

January Makamba

Kupiti ukurasa wake wa Twitter, Makamba amesema kuwa ameyapokea kwa moyo mweupe mabadiliko hayo na atakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia siku zijazo.

Nafasi yake sasa imechukuliwa na George Boniface Simbachawene. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.  Bashe anachukua nafasi iliyoachwa na Mh. Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.