
Mbunge Zitto Kabwe na Kamanda Mambosasa.
Akizungumzia juu ya kauli zilizotolewa na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe juu ya alipo Raphael, kamanda amesema taarifa hizo ni za mitandaoni, na kwamba wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.
"Hizo habari za mitandaoni kila mmoja anatoa, cha msingi sisi tunachokiona kama kuna jambo lolote lipelekwe kituo cha polisi, ofisi yangu ipo, kama kuna mtu ana taarifa alete''
Siku ya Julai Mosi, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, aliahidi kuwasilisha ushahidi wa eneo alilowekwa Raphael, kuanzia siku ya kwanza alipotekwa hadi siku ya Jumamosi.
Raia huyo wa Kenya ambaye ana mke na watoto wawili, alitekwa Juni 24 maeneo ya Oyserbay Dar es salaam ambapo hadi sasa bado hajapatikana.