Wednesday , 28th Oct , 2015

Makandarasi wadogo nchini Tanzania wametakiwa kushirikiana ili walete ushindani na kampuni kubwa katika kupata zabuni za kufanya maendeleo ndani ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Tanzania CRB , Consolata Ngwimba

Wito huo umetolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa bodi ya makandarasi Tanzania CRB , Consolata Ngwimba kwenye mkutano wa zaidi ya makandarasi wadogo elfu 60.

Ngimbwa amesema umuhimu wa makandarasi wadogo kuungana ni kuongeza uwezo wa ufanyaji kazi na kuwa na vigezo vingi ili uweze kupata zabuni kubwa kwa kukidhi viwango kutokana na ushirikiano wao.

Kwa upande wake msajili wa CRB Joseph Malongo amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo makandarasi wadogo ni kuachiwa kazi kubwa na wale wakubwa wanapoingia ubia.