Monday , 7th Apr , 2014

Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine 19 wamejeruhiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fedha baada ya majambazi kufunga barabara kwa Mawe na Magogo na kisha kuteka magari katika eneo la Katadoma barabara ya Morogoro Iringa.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, John Laswai amesema tukio hilo limetokea jana majira ya usiku ambapo Majambazi hao wakiwa na silaha mbalimbali waliteka magari na kujeruhi abiria na kupelekea kifo cha abiria mmoja wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Richard.

Majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakielezea tukio hilo wamesema wao ni madareva wa magari ya IT walikua wakitokea Mbeya kurudi Dar es Salaam wakikutana na foleni kubwa barabarani ndipo wakatekwa na kujeruhiwa ambapo wamekiri kupoteza fedha mali na simu za mkononi.