Wednesday , 7th Sep , 2016

Jaji mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande amesema jumla ya wafanyakazi 34 wa mahakama wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 18 mwezi uliopita.

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman

Jaji Chande amesema kuwa kati ya hao, 11 ni mahakimu wa mahakama mbalimbali huku wengine 23 ni watendaji wa mahakama na maafisa wa mahakama.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi kwa mahakama hapa nchini Mhe. Chande amesema mahakimu hao pamoja na maafisa wa mahakama wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya utovu wa nidhamu.