Tuesday , 10th Feb , 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  amesema ili mahakama zifanye kazi zake kwa uadilifu  na ziendelee kuwa huru mihimili mengine  haipaswi kuingilia  katika maamuzi  yake inayotoa na kutaka itekezwe.

Dkt Shein ametoa kauli hiyo hapa Zanzibar wakati akihutubia katika siku ya sheria Zanzibar ambayo ilifanyika katika viwanja vya  bustani ya Victoria  na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria  wakiwemo majaji, mahakimu, wanasheria na mawakili wakiongozwa na makamu wa pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi pamoja na Jaji mkuu wa Tanzania Omar Chande.

Dkt Shein aliwataka majaji na mahakimu kufanya kazi yao bila ya hofu na bila ya upendeleo huku akiwataka wananchi  kufanya juhudi za kuzielewa  na kuzifuata sheria.

Mapema katika siku hiyo ya sheria Zanzibar wakuu wa sekta  hiyo muhimu za sheria walipata fursa ya kutoa salamu zao ambapo  mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan alisisitiza umuhimu wa Katiba na utawala bora huku Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar Awadh Ali Said alishauri serikali  kuanzisha mfuko maalum wa utendaji wa mahakama.

Naye Jaji mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Makungu kwa upande wake amesema bado tatizo la rushwa limekuwa ni sugu ingawa mahakama imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana nayo.

Sherehe hizo za siku ya sheria Zanzibar ambazo mwaka huu kauli mbiu ni  mahakama huru, msingi na utawala bora