
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Ivan Msack ameridhia ombi la kuwafutia mashtaka washtakiwa hao na hivyo kuhairisha kesi hadi Aprili 24 ambako washtakiwa 13, wakiwemo wabunge wawili Suzan Kiwanga (Mlimba) na Peter Lijualikali wa Kilombero.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera aliwasilisha ombi la kuwafutia mashtaka washtakiwa hao 44 kwa kile walichodai kuwa hawana ushahidi wa nguvu utakaowatia hatiani washtakiwa hao.
Mawakili upande wa utetezi umeweka wazi kuwa wanajiandaa kukabiliana na ushahidi utakaotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya wabunge hao na wengine 11.