Wednesday , 29th Jun , 2016

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemwamuru msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Rungwe, kumkabidhi hati ya Ushindi Mbunge wa Jimbo hilo Saul Amon kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemwamuru msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Rungwe, kumkabidhi hati ya Ushindi Mbunge wa Jimbo hilo Saul Amon kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kutupilia mbali madai ya kupinga matokeo ya ubunge yaliyotolewa na aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mwambigija.

Mwambigija, alifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kupinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi Mgombea wa CCM, Saul Amon,huku akiorodhesha kasoro mbalimbali zilizokuwa zimeibuka katika uchaguzi huo.

Katika kesi namba mbili ya mwaka 2015 Mwambigija alikuwa
anawakilishwa na Mawakili wawili ambao ni, Benjamini Mwakagamba na Adrian Mhinaambao waliwasilisha hoja 13 mahakamani za kupinga matokeo hayo.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Barke Sahel, wa Kanda ya Dodoma amesema kuwa hoja za mlalamikaji hazina mashiko yanayoweza kuifanya Mahakama hiyo kubadili matokeo ya uchaguzi na hivyo akamtangaza, Amon Saul, kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Rungwe na kumuagiza Msimamizi wa Uchaguzi kumkabidhi Hati ya Ushindi.

Hata hivyo Jaji Sahel, katika Hukumu hiyo amesema kuwamlalamikaji katika Kesi hiyo ambaye ni John Mwambigija, wa CHADEMA atatakiwa kurejesha gharama za uendeshaji wa kesi hiyo na kwamba ana uhuru wa kukata rufaa.