Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Tanzania, Mohammed Mpinga.
Vifo hivyo vimetokana na ajali laki moja, elfu tisini na tisa na mia sita arobaini na nane ambapo jumla ya watu laki moja na elfu sabini na tano, mia moja sabini na tano wamejeruhiwa.
Mwaka mbaya kuliko yote kwa mujibu wa takwimu hizo ni mwaka 2013 ambapo jumla ya watu 4002 walifariki kutokana na ajali za barabarani, huku wengine 20,689 wakipata majeraha katika sehemu mbali mbali za miili yao.
Hata hivyo mwaka huu huenda hali ikawa tofauti kwani kati ya Januari na sasa watu waliofariki kwa ajali ni 1743 katika ajali 8405 huku waliojeruhiwa wakiwa ni watu elfu saba.