Akiongea katika uzinduzi wa bodi mpya ya utalii TTB Prof. Jumanne Magembe amesema ni vyema bodi hiyo ikatanguliza weledi na taaluma mbele katika kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inchini inakuwa kimataifa na kuepuka kuingia mikataba mibovu ambayo inarudisha nyuma juhudi za sekta hiyo.
Magembe amesema kwa sasa Tanzania inalenga kuboresha huduma zake za usafiri wa anga ambapo miezi ya hivi karibuni ndege mpya zitanunuliwa ili kuhakikisha kuwa safari za anga nchini zinachangia ukuaji wa sekta ya utalii.
"Ndege mpya zitawasili nchini mwezi ujao, hii nifursa kwetu sisi, Bodi mchangamkie kuhakikisha safar
Aidha Prof. Magembe ameongeza kuwa kwa sasa watalii milioni moja pekee hutembelea Tanzania kwa mwaka idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na nafasi ya Tanzania kiutalii duniani hivyo kuwataka wakurugenzi wapya wa bodi hiyo kuhakikisha Tanzania inafikisha watalii milioni 3 ifikapo mwaka 2020.




