Friday , 15th Jan , 2016

Viwanda vingi nchini vimekufa na kuacha kuendelea kuzalisha na kuuza mali kutokana na ubadilikaji wa masoko ya nje, ukosefu wa mali ghafi na sera zetu nyingi zinazotungwa hazizingatii kuinua viwanda.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe wakati akizungumzia dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutaka kuvichukua viwanda ambavyo havizalishi kwa muda mrefu hivyo wameiomba serikali iweke dhamira na sera itakayowasaidia wazalishaji kuzalisha na kuuza.

Amesema sera hiyo iwe endelevu na isaidie kulinda viwanda vilivyopo na kuhamasisha watu waingie katika uzalishaji ambao utaweza kupunguza bidhaa nyingi kutoka nje na kuon geza pato la taifa.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye viwango na ubora unaotambulika kimataifa.