Wednesday , 4th Nov , 2015

Serikali imesema kuwa maandalizi ya sherehe ya kumwapisha Rais mteule wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli yamekamilika na wageni waalikwa wameshaanza kuwasili nchini.

Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asah Mwambene

Msemaji wa serikali na mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asah Mwambene amesema kuwa Kila kitu kinaenda vizuri na baadhi ya viongozi hao waalikwa wakiwemo marais na viongozi waandamizi na mashirika ya kimataifa toka nchi mbalimbali wameanza kuwasili na wengine wanaendelea kuwasili leo mchana.

Mwambene ameongeza kuwa serikali pia inatoa pongezi kwa vyombo vya habari kwa kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuripoti habari za uchaguzi bila kuwagawa watanzania na kusisitiza amani na kusaidia uchaguzi kufanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Wakati huo huo Asah Mwambene amekanusha taarifa mbalimbali za uvumi wa kifo cha Rais wa awamu ya tatu Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa kuwa ni mzima wa Afya na kesho atahudhuria katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais mteule John Magufuli.